Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Habari la Muqawama wa Kiislamu wa Iraq, Kataib Sayyid al-Shuhada, umetoa taarifa kwa vyombo vya habari ukisema: "Muqawama wa Kiislamu wa Iraq, Kataib Sayyid al-Shuhada, unapinga kauli zisizo sahihi zilizotolewa na Fuad Hussein, na unasisitiza kuwa Kataib Sayyid al-Shuhada al-Mansurah imesaini hati ya makubaliano kuhusu mamlaka na uhuru wa Iraq. Hati hiyo ilisainiwa na makundi manne ya Muqawama, sambamba na wawakilishi wa Muungano wa Mfumo wa Uratibu (Al-Ittar al-Tansiqi) pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu.
"Kundi hili bado linazingatia masharti ya makubaliano hayo. Hadi sasa, halijatangaza wala kuchukua msimamo wowote kuhusu silaha zake, wala halijasaini makubaliano yoyote yanayohusu suala hilo.
"Kwa kusisitiza ukweli huu, tunawaomba wasemaji wote, hususan viongozi wa serikali ambao wanatarajiwa kuwa makini zaidi kuliko wengine katika kuhakikisha usahihi wa taarifa, kuzingatia umakini na uwajibikaji wanapowasilisha taarifa na kutoa kauli zao, ili kuzuia kuzuka mkanganyiko au kuifikishia jamii taarifa zisizo sahihi.
"Katika muktadha huo huo, tunakubali udhuru wa ndugu yetu Fuad Hussein, kwa kuwa amekuwa mbali na uhalisia wa matukio na hana ufahamu wa kutosha kuhusu yanayotokea katika uwanja wa mapambano na hali halisi iliyopo nchini, hali hii inatokana na safari zake nyingi na uwepo wake mdogo mjini Baghdad.
"Vilevile, tunatangaza utayari wetu wa kumpatia taarifa na ufafanuzi maalumu kwa vipindi maalumu kuhusu maendeleo na matukio mbalimbali yanayotokea nchini Iraq, ili apate kuufahamu ukweli, aendelee kufuatilia maendeleo ya mambo na kuepuka kujikuta katika makosa ya aina hii hapo baadaye."
Baraza la Habari la Muqawama wa Kiislamu wa Iraq
Kataib Sayyid al-Shuhada al-Mansurah
7 Oktoba 2026 (sawa na 16 Aban 1405 Hijria Shamsia).
Ikumbukwe kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein, jana Jumamosi, katika mahojiano na televisheni ya Al-Jazeera, alidai kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo amefikia makubaliano na makundi manne yenye silaha, yakiwemo Asa'ib Ahl al-Haq na Vikosi vya Sayyid al-Shuhada, kuhusu suala la kuweka utaratibu wa kudhibiti silaha, aliongeza kuwa mazungumzo na makundi mengine bado yanaendelea.
Maoni yako